rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Palestina Israeli Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Maelfu ya Wapalestina waandamana karibu na mpaka wa Israel

media
Maandamano ya Wapalestina katika mpaka wa Israel REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa

Maelfu ya Wapalestina, wameandama karibu na mpaka wa Israel kuadhimisha mwaka mmoja, baada ya mapigano katika ukanda wa Gaza.


Wapalestina wanawakumbuka wenzao zaidi ya 200 waliouawa baada ya mapigano ya siku kadhaa kati ya wapiganaji wa kundi la Hamas na wanajeshi wa Israel.

Wakati wa maandamano ya leo, Mpalestina mmoja aliuawa baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israeli.

Waandamanaji waliokuwa wanaimba nyimbo za kulaani Israeli, waliwarushia mawe wanajeshi wa Israeli ambao walilazimika kuwashambulia.

Maandamano haya yamekuka, siku 10 kuelekea Uchaguzi wa Israeli lakini pia umekuja, baada ya Misri siku chache zilizopita, kuwezeha kupatanisha kundi la Hamas na Israel kuhusu eneo la ukanda wa Gaza