Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-ISRAELI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Uhuru wa Israeli kuhusu Milima ya Golan: Saudi Arabia yalaani msimamo wa Marekani

Saudi Arabia imeshutumu uamuzi wa Donald Trump kutambua uhuru wa Israeli kuhusu Milima ya Golan kama ukiukwaji wa mkataba wa kimataifa na azimio la kimataifa.

Rais wa Marekani Donald Trump akisaini sheria inayotambua uhuru wa Israeli kuhusu eneo la Milima ya Golan, Machi 25, 2019 White House, Washington.
Rais wa Marekani Donald Trump akisaini sheria inayotambua uhuru wa Israeli kuhusu eneo la Milima ya Golan, Machi 25, 2019 White House, Washington. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia imefutilia mbali uamuzi huo na kulani tangazo la utawala wa Marekani kutambua uhuru wa Israeli kuhusu Milima ya Golan upande wa Syria inayokaliwa na Wayahudi," shirika la Habari la SPA limeripoti.

Golan itabaki kiuwa ardhi ya Syria "inayokaliwa na Wayahudi" na kutambua eneo hilo kama sehemu ya ardhi ya Israeli ni "ukiukwaji mkubwa wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa na azimio la kimataifa," Saudi Arabia imeongeza.

"Kutakuwa na athari mbaya juu ya mchakato wa amani katika Mashariki ya Kati, pamoja na usalama na utulivu katika ukanda huo," taarifa ya Saudi Arabia imebaini.

Israeli ilitawala sehemu kubwa ya kubwa ya eneo la Golan nchini Syria (kilomita mraba 1,200) wakati wa Vita ya Siku sita mnamo mwaka 1967, kabla ya kulifanya kuwa moja ya sehemu zake za ardhi mnamo mwaka 1981. Eneo hilo halijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.