Pata taarifa kuu
SYRIA-ISRAELI-MAREKANI-USHIRIKIANO-USALAMA

Miji kadhaa ya Syria yakumbwa na maadamano dhidi ya uamuzi wa Marekani

Wananchi wa syria kutoka miji mbalimbali yamemiminika mitaani leo Jumanne kupinga uamuzi wa Marekani wa kutambua uhuru wa Israel kuhusu eneo lenye Milima la Golan.

Picha ya rais wa Syria Bashar al-Assad na bendera ya Syria katika mji wa Quneitra katika eneo la Milima la Golan Machi 26, 2019.
Picha ya rais wa Syria Bashar al-Assad na bendera ya Syria katika mji wa Quneitra katika eneo la Milima la Golan Machi 26, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu rais wa Marekani Donald Trump alisaini sheri inayotambua uhuru wa Israeli kuhusu eneo la Golan. sherhe hiyo ilifnyiks kstiks ikulu ys White House mbele ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye alikuwa ziarani nchini Marekani.

Eneoa lenye milima la Golan linakaliwa na Wayahudi tangu mwakaa 1967 na Israeli ilifanya eneo hilo kama moja ya sehemu zake za ardhi mnamo mwaka 1981.

Lakini mpaka sasa eneo hilo halijatambuliwa na jumuiya ya kimataifa kama sehemu ya ardhi ya Israeli.

Wachambuzi wa masuala ya kidiplomasia wanasema eneo la Golan linakaliwa kimabavu na baadhi ya raia wa Israeli.

Maandamano hayo yamefanyika katika miji mbalimbali, hususan Homs (katikati mwa nchi), Qamishli na Hasaka, kaskazini mwa nchi eneo linalodhibitwa na Wakurdi, Aleppo (kaskazini mwa nchi), Deir Ezzor (mashariki mwa nchi) na katika mji mkuu Damascus na katika maeneo yenye wafuasi wengi wa rais Bashar al-Assad huko Latakia na Tartous (magharibi),kwa mujibu wa shirika la Habari la serikali la Sana.

Waandamanaji wameshikilia picha ya rais Bashar al-Assad na bendera za Syria na Palestina, chanzo hicho kimesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.