rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Kumi na tatu wauawa katika mashambulizi ya angani Afghanistani

media
Miili ya watoto wadogo waliouawa katika mashambulizi ya angani ikiwekwa kwenye lori Machi 23, 2019 karibu na mji wa Kunduz. © AFP

Watu,ikiwa ni pamoja na watoto 10, waliuawa katika mashambulizi ya angani yaliyoendeshwa na muungano wa majeshi ya kimataifa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi ambapo raia wameendelea kulengwa.


"Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan umeelezea huzuni wake , kulingana na uchunguzi watu kumi miongoni mwa watu waliouawa walikuwa ni kutoka familia moja waliotoroka makazi yao kufuatia kuuka kwa mapigan kwingineko nchini," Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (Manua) umesema katika taarifa yake.

Mbali na majeshi ya Afghanistan, majeshi ya Marekani pekee ndio yanafanya operesheni zakijeshi na mashambulizi ya angani nchini humo.

Msemaji wa ujumbe wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) nchini Afghanistan ameliambia shirika la Habari la AFP kuwa uchunguzi unaendelea.

Kwa mujibu wa Manua, "tukio hilo lililotokea katika wilaya ya Telawka, karibu na mji wa kaskazini wa Kunduz, wakati wa operesheni iliyokuwa ikiendeshwa na vikosi vya serikali dhidi ya wapiganaji wa taliban katika eneo hilo.

Watu watatu pia walijeruhiwa, kwa mijibu wa Umoja wa Mataifa."Wale waliouawa walikuwa ni kutoka familia moja ambao walitoroka makazi yao kufuatia kuzuka kwa mapigano katika wilaya ya Dashte Archi" Kaskazini ya mji mkuu wa mkoa, "na ambao hivi karibuni waliwasili katika mji huo," Khosh Mohammad Nasratyar, afisa wa serikjali ya mkoa wa Kunduz ameliambia shirika la Habari la Kunduz.