Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-UN-KHASHOGGI-HAKI

Mauaji ya Khashoggi: Umoja wa Mataifa washtumu utawala wa kifalme wa Saudia

Katika taarifa yake, Agnes Callamard, kiongozi wa maafisa wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ameshtumu utawala wa Kifalme wa Saudi Arabia kuhusika na kifo cha mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.

Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Kifalme wa Saudi Arabia, aliuawa Oktoba 2 katika majengo ya ubalozi mdogo wa Saudi, Istanbul.
Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Kifalme wa Saudi Arabia, aliuawa Oktoba 2 katika majengo ya ubalozi mdogo wa Saudi, Istanbul. AFP/Mohammed Al-Shaikh
Matangazo ya kibiashara

Jamal Khashoggi aliuawa Oktoba 2, 2018 katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia, jijini Istanbul, nchini Uturuki.

Maafisa wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa wamebaini kwamba mauaji ya Jamal Khashoggi "yalipangwa" na utawala wa Saudi Arabia na ni "ukiukwaji mkubwa wa haki ya msingi kuliko nyingine, haki ya kuishi".

Pia Agnes Callamard amelaani matumizi ya "kinga" ya kidiplomasia kufanya mauaji ya "kikatili".

"Ushahidi uliokusanywa wakati wa ziara yangu nchini Uturuki unaonyesha ... kwamba Bw Khashoggi, mauaji yake ya kikatili yalipangwana wawakilishi wa utawala wa Kifalme wa saudi Arabia," amesema Agnes Callamard, akinukuliwa katika taarifa hiyo.

Zaidi ya miezi minne baada ya kifo chake, mwili wa mwandishi wa habari wa Washington Post, bado haujapatikana. Mauaji yake yaliitumbukiza Saudi Arabia katika mogogoro mkubwa wa kidiplomasia na kuchafua jina la mwanamfalme Mohammed bin Salman ambaye anashtumiwa na maafisa wa Marekani na Uturuki kutoa agizo kwa mauaji hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.