rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

Syria Uturuki

Imechapishwa • Imehaririwa

Syria: Wapiganaji 400 wa Kikurdi waondoka Manbij

media
Waasi wa Syria waliungwa mkono na Uturuki katika mkoa wa Manbij, Desemba 29, 2018 (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Khalil Ashawi

Jeshi la Syria limetangaza kwamba wapiganaji 400 wa Kikurdi wameondoka katika mji wa Manbij, Kaskazini mwa Syria tangu Jumatano Januari 2, 2019. Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya kutumwa kwa wanajeshi wa Syria katika eneo hilo kwa wito wa vikosi vya Kikurdi vinavyotishiwa na mashambulizi kutoka Uturuki.


Takribani magari 30 yaliyokuwa yakibeba wapiganaji 400 wa Kikurdi yaliondoka katika mji wa Manbij siku ya Jumatano. Video iliyorushwa kwenye mtandao wa You Tube inaonyesha msafara wa magari ya wapiganaji wa Kikurdi yakiondoka mji huo na kwenda upande wa pili wa mto.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Syria, kundi lingine la wapiganaji wa Kikurdi linatarajiwa kuondoka katika mji huo katika saa chache zijazo.

Hatua hiyo ya kuondoka kwa wapiganaji wa Kikurdi katika mji wa Manbij inakuja wakati jeshi la Syria linaendelea kutuma wanajeshi wengi kaskazini mwa Mmji huo, ambako waasi wanaounga mkono majeshi ya Uturuki wamekusanyika baada ya vitisho vya serikali ya Ankara kuanzisha operesheni kabambe ya kuwatimua wanamgambo wa Kikurdi, ambao Uturuki inawataja kama magaidi.

Kufuatia makubaliano na Damascus ili kuepuka mashambulizi ya Uturuki, Wakurdi walikubali kutumwa kwa jeshi la Syria katika mji wa Manbij na kurudi kwa utawala chini ya udhibiti wa serikali kuu ya Damascus.

Jeshi la Syria sasa limepiga kambi kaskazini na kaskazini magharibi mwa Manbij. Linatarajia kuingia katika mji huo mara tu vikosi vya Kikurdi na askari wa mwisho wa Marekaniwanakuwa wameondoka.