Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Shambulizi Kabul: Idadi ya waliouawa yaongezeka na kufikia 43

Shambulizi la siku ya Jumatatu katika jengo moja la serikali katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul, ulioshambuliwa kwa muda wa saa saba na watu wenye silaha, limegharimu maisha ya watu 43 na 10 kujeruhiwa, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Afghanistan Jumanne wiki hii.

Mtu aliyejeruhiwa akifikishwa hospitali ya Wazir Akbar Khan baada ya mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari Kabul Desemba 24, 2018.
Mtu aliyejeruhiwa akifikishwa hospitali ya Wazir Akbar Khan baada ya mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari Kabul Desemba 24, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hili ni shambulizi baya zaidi kutokea katika mji wa Kabul tangu mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua mwezi uliyopita katika mkutano wa viongozi wa kidini wa ngazi ya juu na kuua watu wasiopungua 55.

Shambulizi hili limetokea baada ya tangazo ambalo halikuthibitishwa rasmi la kuondoka hivi karibuni kwa askari 7,000 wa Marekani kati ya 14,000 waliopo Afghanistan. Hatua ambayo mmoja wa wakuu wa kijeshi wa Taliban amekaribisha.

Shambulio dhidi ya jengo la serikali, kunakopatikana Wizara ya Ujenzi na Kazi na Wizara ya Jamii, lilidumu saa zaidi ya saba. Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo mara moja.

Waathirika wengi ni raia wa kawaida, msemaji wa wizara ya Afya, Najib Danish, amesema.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan viliua watatu miongoni mwa washambuliaji wanne na kuokoa watu zaidi ya 350 waliokuwa wamekwama katika jengo hilo, Danish ameongeza.

Mshambuliaji wa nne aliuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari, kabla ya shambulio hilo kuanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.