Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-USALAMA

Syria: makaburi Saba ya halaiki yagunduliwa Boukamal

Makaburi Saba yaliyokuemo zaidi ya miili mia moja ya watu wasiojulikana imegunduliwa karibu na mji wa Boukamal, ngome ya zamani ya kundi la Islamic State (IS), mashariki mwa Syria, shirika la Habari la SANA limeripoti.

Wataalamu wakichunguza kaburi la halaiki Boukamal, mashariki mwa Syria, kulingana na picha ya shirika la Habari la Syria SANA, Desemba 11, 2018.
Wataalamu wakichunguza kaburi la halaiki Boukamal, mashariki mwa Syria, kulingana na picha ya shirika la Habari la Syria SANA, Desemba 11, 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mamlaka husika zimegundua makaburi Saba ya ambapo kumepatikana miili zaidi ya mia moja ya watu wasiojulikana," shirika hilo limesema, huku likishtumu kundi la IS kuwa lilihusika katika mauaji hayo.

"Kikosi cha Ulinzi wa raia na shirika la kihisani la Msalaba Mwekundu wamegundua miili 101 ya watu waliouawa, ambapo wengi walifanyiwa mateso na matendo na unyanyasaji kabla ya kuuawa," limesema shirika la Habari la SANA, likibaini kwamba operesheni inaendelea kwa kutoa "miili zaidi "katika mji huo wa mkoa wa Deir Ezzor, mashariki mwa nchi.

Timu zilizo kwenye eneo la tukio zinaendelea na zoezi la "utambuzi wa miili ambayo tayari imepatikana, ambapo baadhi ni ya wanawake," chanzokutoka shirika la Msalaba Mwekund ambacho hakikutaja jina kimeliambia shirika la Habari la AFP.

Machafuko nchini Syria yaliyozuka mnamo mwaka 2011, yamesababisha zaidi ya watu 360,000 kupoteza maisha na mamilioni ya watu kuyatoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.