Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Waasi wa Houthi: Tuko tayari kusitisha mapigano kama Riyad inataka amani

Hatimaye waasi wa Houthi nchini Yemen wametangaza rasmi kwamba wako tayari kusitisha mashambulizi ya aina yoyote dhidi ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kirabu (UAE), kulingana na taarifa iliyotolewa usiku wa manane Jumapili Novemba 18.

Makundi yanayosaidia majeshi ya serikali yakikusanya katika vitongoji vya Hodeida tarehe 9 Novemba 2018 (picha ya kumbukumbu).
Makundi yanayosaidia majeshi ya serikali yakikusanya katika vitongoji vya Hodeida tarehe 9 Novemba 2018 (picha ya kumbukumbu). STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waasi hawa wa Kishia wanaoungwa mkono na Iran wamesema wako tayari kukubali kusitisha mapigano kama muungano wa nchi zenye madhehebu ya Kisuni, unaoongozwa na Saudi Arabia "unataka kweli amani".

Tangazo hilo la waasi wa Kihouthi linatokana na kushindwa kudhibiti mashambulizi ya kijeshi muungano wa Kirabu unaongozwa na Saudi Arabia. Muungano ambao tangu mwanzo wa mapigano mwaka 2015 umedhibiti bandari zote za Yemen kutoka mikononi mwa waasi wa Kihouthi. Hodeida kwenye Bahari Nyekundu, ambayo ni bandari ya mwisho inayoshikiliwa na waasi, kwa sasa inahatishiwa na vikosi vya muungano ambao umedhibiti kusini na mashariki mwa jiji hilo.

Hata hivyo waasi wa Kihouthi wanasema wako tayari kutafuta wapiganaji zaidi ili kupambana, kudhibiti ngome yao muhimu ya mji wa Hodeida.

Kwa wiki kadhaa sasa, mapigano makali yamekuwa yakiendelea kati ya waasi hao na muungano wa jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia, kudhibiti mji huo ambao una bandari muhimu.

Tangazo hili la waasi limekuwa wakati huu Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths akitarajiwa kuwasili jijini Sanaa, kujaribu kushawishi pande zinazopigana kuja kwenye meza ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.