Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAREKANI-JAMAL-HAKI

Kesi ya Jamal Khashoggi: Polisi ya Uturuki yaendesha msako

Polisi ya Uturuki inaendesha msako katika misitu ulio pembezoni mwa mji wa Istanbul na katika mji ulio karibu na Bahari ya Marmara kama sehemu ya uchunguzi wa kutoweka kwa Jamal Khashoggi.

Raia huyo akishikilia bango linaloandikwa "yuko wapi Jamal Khashoggi? Wakati wa maandamano ya kuunga mkono mwandishi huyo wa habari,  mkosoaji mkubwa wa utawala wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi, Istanbul tarehe 9 Oktoba 2018.
Raia huyo akishikilia bango linaloandikwa "yuko wapi Jamal Khashoggi? Wakati wa maandamano ya kuunga mkono mwandishi huyo wa habari, mkosoaji mkubwa wa utawala wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi, Istanbul tarehe 9 Oktoba 2018. OZAN KOSE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi huyo wa habari wa gazeti la Washington Post kutoka Saudi Arabia alitoweka tangu alikwenda katika ubalozi wa nchi yake mjini Istanbul Oktoba 2, 2018. Serikali ya Uturuki inasema uchunguzi wake unaendelea na kupatikana kwa mwili wa mwandishi huyo itakuwa ni hatua kubwa, wakati uvumi umeendelea kusambaa katika maeneo mbalimbali nchi Uturuki na Saudi Arabia.

Tangu mwanzo wa uchunguzi wa kutoweka kwa Jamal Khashoggi, serikali ya Uturuki imekuwa ikisema kuwa, mwandishi huyo wa habari aliuawa katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, katika mazingira ya kutatanisha.

Hayo yanajiri wakati Rais wa Marekani  Donald Trump amesema inavyooneka, Mwanahabari wa Saudi Arabia Jamal Khashoogi aliyetoweka akiwa ndani ya Ubalozi wa nchi yake, nchini Uturuki, ameuawa.

Trump amesema inasikitisha sana lakini anasubiri ripoti kamili kabla ya kutangaza hatua ambazo amesema zitakuwa kali kwa uongozi wa Saudi Arabia.

"Nafikiri ameuawa, inasikitisha sana, lakini tunasubiri matokeo ya uchunguzi, kufahamu kilichotokea," alisema Trump.

Khashoogi alionekana akiingia kwenye ubalozi wa nchi yake jijini Instanbul, lakini hakuonekana tena.

Saudi Arabia imekanusha kuhusika na madai ya kuuawa kwa Mwanahabari huyo ambaye amekuwa akiandika makala za kuukosoa uongozi wa Riyadh.

Marekani inasema itaichukulia hatua kali Saudi Arabia iwapo itabainika kuwa ilihusika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.