Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-USALAMA

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura aachia ngazi

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura ametangaza kuwa atajiuzulu kufikia mwisho wa mwezi Novemba. Mistura ambaye ana umri wa miaka 71, anakuwa mjumbe wa tatu kujiuzulu kuhusu vita vya Syria.

Baada ya miaka minne na miezi minne, Staffan de Mistura anajiuzulu kwenye nafasi ambayo baadhi wanaona kama "kazi ngumu zaidi duniani".
Baada ya miaka minne na miezi minne, Staffan de Mistura anajiuzulu kwenye nafasi ambayo baadhi wanaona kama "kazi ngumu zaidi duniani". Fabrice COFFRINI / AFP
Matangazo ya kibiashara

De Mistura, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka minne sasa kuwa ameona vema aachane na kazi hiyo ngumu ya kusaidia kurejesha amani nchini Syria kutokana na vita vya miaka saba ambavyo hadi sasa haijafahamika vitaisha lini.

Lakini katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York, De Mistura amesema anajiuzuku ili awe na muda na familia yake.

"Sababu za kibinafsi za kujiuzulu si afya, ni familia kimsingi. Mimi ni mzima sina neno na hata sijachoka, kwa sababu kazi hii imekuwa ikinitia tumbo joto," amesema de Mistura .

De Mistura ndiye mpatanishi aliyehudmu kwa muda mrefu zaidi kati ya wapatanishi watatu wa Umoja wa Mataifa waliohudumu wakati wa zaidi ya miaka saba ya mzozo wa Syria. Watangulizi wake, katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, marehemu Kofi Annan na mwanadiplomasia mkongwe kutoka Algeria Lakhdar Brahimi, wote walijiuzulu baada ya kukatishwa tamaa kutokana na mkwamo wa kimataifa kuhusu jinsi ya kuvifikisha mwisho vita nchini Syria

De Mistura, raia wa Italia mwenye asili ya Uswisi alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha mchakato wa kisiasa unaendelea nchini Syria.

Watu wanaofikriwa huenda wakajaza pengo litakaloachwa na de Mistura ni mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Jan Kubis, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Algeria, Ramtane Lamamra, mjumbe wa Umoja wa Mataia kwa ajili ya Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov na balozi wa Norway nchini China, Geir Pedersen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.