Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAREKANI-JAMAL-HAKI

Kesi ya Khashoggi: Mike Pompeo awasili Ankara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo anewasili mjini Ankara nchini Uturuki, na anatarajia kukutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mevlut Cavusoglu.

Polisi wa Uturuki wakifanya msako katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia Istanbul, Uturuki, tarehe 15 Oktoba.
Polisi wa Uturuki wakifanya msako katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia Istanbul, Uturuki, tarehe 15 Oktoba. Bulent KILIC / AFP
Matangazo ya kibiashara

Bw Pompeo anawasili Ankara wakati vyombo vya habari vya serikali vikichapisha taarifa mpya zinazoishtumu Suadi Arabia kuhusika katika mauaji ya mwandishi wa habari wa gazeti la Washington Post jamal Khashoggi.

Taarifa hizo zinaelezea mateso na mauaji vilivyoendeshwa na maafisa wa Saudi Arabia dhidi ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi katika ubalozi wa nchi hiyo mjini Istanbul tarehe 2 Oktoba, 2018.

Hayo yanajiri wakati Rais wa Marekani Donald Trump amebadili kauli akisema kuwa Saudi Arabia ichukuliwe kama haina hatia katika kesi hiyo.

Kauli hii inakuja siku chache baada ya Rais trump kuomba uchunguzi ufanyike akiishtumu Saudi Arabia kuhusika na kisa hicho.

Hivi karibuni Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliitaka Saudia kutoa ushahidi kuhusiana na mwandishi wa habari aliyepotea kwamba alitoka nje ya majengo ya ubalozi wao mjini Istanbul.

Mwanadishi huyo wa habari alitoweka Jumatano wiki mbilizi zilizopita baada ya kwenda katika ubalozi wa Saudi Arabia huko Istanbul, nchini uturuki, ambako alikuwa alikuja kutafuta vibali vya ndoa kati yake na mchumba wake raia wa Uturuki, Hatice Cengiz, kufuatia kuvunjika kwa ndoa yake ya awali. Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari kutoka Saudi Arabia, mkosoaji mkubwa wa utawala wa kifalme nchini hmu, aliitoroka nchini yake mwaka jana na kukimbilia nchini Marekani kwa hofu ya kukamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.