Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-MASHAMBULIZI

Marekani yaonya dhidi ya kuushambulia mkoa wa Idlib kwa silaha za kemikali

Marekani imesema italazimika kutumia nguvu dhidi ya serikali ya Syria iwapo itavamia mkoa wa Idlib kwa kutumia silaha za kemikali. 

Mji wa Idlib nchini Syria
Mji wa Idlib nchini Syria Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa juu wa jeshi nchini humo Jenerali Joseph Dunford amesema, hakuna uamuzi ambao umeshafanyika lakini mashauriano na rais Donald Trump yanaendelea.

Syria inasema haijawahi kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

Siku ya Ijumaa, viongozi kutoka Urusi, Uturuki na Iran, walishindwa kuafikiana kuhusu namna ya kutekeleza mashambulizi katika ngome hiyo ya mwisho ambayo bado inashikiliwa na wapinzani wa rais Bashar Al Assad.

Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa, Urusi ambayo inaunga mkono mashambulizi ya jeshi katika eneo hilo, imetekeleza mashambulizi ya angaa na kusababisha vifo vya watu watano.

Rais Vladimir Putin ambaye ameendelea kuwa mshirika wa karibu wa rais Assad, anataka jeshi la Syria liruhusiwe kudhibiti ngome ya Idlib ambayo ndio inayosalia kuwa mikononi mwa wapinzani wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.