Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-USALAMA

Ndege za kijeshi za Urusi zaendesha mashambulizi Idlib

Ndege za kivita za Urusi zimefanya mashambulizi ya anga dhidi ya mkoa wa Idlib, unaoshikiliwa na wapiganaji kaskazini magharibi mwa Syria, baada ya siku 22 mapigano kusitishwa, shirika la HAki z Binadamu (OSDH), limebaini.

Urusi yaendesha mashambulizi ya anga Idlib.
Urusi yaendesha mashambulizi ya anga Idlib. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Urusi inasaidia kijeshi serikali ya Rais Bashar al-Assad, ambapo jeshililiendesha mashambulizi ya anga dhidi ya mkoa huo.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov amesema kuwa eneo la Idlib ni "kiota cha magaidi" wkinachohatarisha mchakato wa amani nchini Syria na kutumika kama ngome kuu kwa kuandaa mashambulizi dhidi ya vikosi vya Urusi nchini. .

Wiki iliyopita, chanzo kilio karibu na serikali ya Damascus kilisema kwamba serikali ya Syria inanijiandaa kufanya mashambulizi kwa minajili ya kurjesha kwenye himaya yake mkoa wa Idlib, lakini Uturuki, ambayo jeshi lake lina mlolongo wa vituo vya uchunguzi katika eneo linaloshikiliwa na waasi, ilionya dhidi ya kampeni hiyo ya kijeshi.

Jumatatu usiku, Rais wa Marekani Donald Trump pia alitoa wito kwa Syria na washirika wake, Iran na Urusi, kutoendesha mashambulizi dhidi ya mkoa wa Idlib, ambao ni ngome kubwa ya mwisho ya waasi nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.