Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA-SIASA

Syria: Marekani na washirika wake waalikwa na De Mistura Geneva

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, ametoa wito kwa Marekani, Ufaransa na nchi nyingine tano kushiriki mazungumzo mjini Geneva tarehe 14 Septemba.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura REUTERS/Pierre Albouy
Matangazo ya kibiashara

Mwaliko huo unakuja siku mbili baada ya De Mistura kukutana na wajumbe wa Urusi, Uturuki na Iran , amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa Jumanne wiki hii.

"Hii itakuwa fursa ya kujadili njia za kendeleza mchakato wa amani," amesema Alessandra Vellucci.

Staffan de Mistura alitoa wito kwa Iran, Urusi na Uturuki kushiriki mazungumzo tarehe 11 na 12 Septemba mjini Geneva kuhusu suala la kuundwa kwa tume itakayohusika nakutunga rasimu ya katiba mpya ya Syria.

Mnamo Septemba 14, anatazamia kukutana na wawakilishi waandamizi wa Marekani, Uingereza, Saudi Arabia, Jordan, Ujerumani, Ufaransa na Misri, amesema Alessandra Vellucci.

Mazungumzo kama hayo na makundi mawili nchi Syria- isipokuwa Misri - tayari yalifanyika mnamo mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.