rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Pakistani Taliban Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 20 waangamia katika shambulizi la kujitoa mhanga Pakistani

media
Pakistan yaendelea kukumbwa na mashambulizi mbalimbali ya Taliban. © AFP

Watu wasiopungua 20, ikiwa ni pamoja na mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa, Haroon Bilour, waliuawa usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii katika shambulio dhidi ya mkutano wa uchaguzi.


Kundi la Taliban limedai kuhusika na shambulizi hilo kwa mujibu wa maaisa wa usalama nchini Pakistani.

Shambulizi hili lililotokea katika Peshawar kaskazini-magharibi mwa Pakistani, nni shambulizi baya lililosababisha vifo vya watu wengi nchini humo tangu kuanza kwa kampeni ya uchaguzi wa wabunge, uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 25.

Shambulizi hili lilitekelezwa wakati wa mkutano wa chama cha Awami National Party (ANP), ambacho tayari kililengwa na mashambulizi ya wapiganaji wa Kiislamu kwa kuonyesha upinzani wake kwa makundi kama vile Taliban.

"Idadi ya watu waliouawa imeongezeka na kufikia 20 na 63 walijeruhiwa, ambapo 35 bado wamelazwa katika hospitali mbili huko Peshawar," mkuu wa polisi Qazi Jameel ameliambia lro Jumatano shirika la habari la AFP.

Idadi hii imethibitishwa na afisa katika Hospitali ya Peshawar, Zulfiqar Babakhel.

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha kutegua mabomu, Shafqat Malik, mshambuliaji wa kujitoa mhanga, 16, alikuwa amebeba kilo 8 ya mabomu na kilo 3 ya vifaa vingine vya kulipuka.