Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Waasi sabini wauawa kusini mwa Syria

Jeshi la Syria, likisaidiwa na jeshi la Urusi, limefaulu kuzima mashambulizi ya waasi katika eneo la kusini linalokabiliwa na machafuko, na kuua karibu wapiganaji 70, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imetangaza Jumatatu wiki hii.

Vikosi vya serikali ya Syria vikiendesha mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa IS katika wilaya ya Hajar al-Aswad, Mei 14, 2018.
Vikosi vya serikali ya Syria vikiendesha mashambulizi dhidi ya ngome za wapiganaji wa IS katika wilaya ya Hajar al-Aswad, Mei 14, 2018. Handout / SANA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya serikali ya Bashar al-Assad yalizindua mashambulizi ili kujaribu kudhibititi eneo linaloshikiliwa na waasi kusini-magharibi mwa Syria, kwenye mpaka na mlima wa Golan karibu na na Israeli na Jordan.Hivi karibuni Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema, hakuna wa kuliagiza jeshi la nchi yake kuondoka nchini Syria kwa sasa. Hata hivyo, alisema Urusi haina mpango wa kujenga kituo cha kudumu cha kijeshi nchini Syria.

Putin aaliongeza kuwa jeshi lake limepata uzoefu wa kipekee nchini Syria na kusisitiza kuwa kuwepo kwao katika nchi hiyo ni kutekeleza majukumu yao ya Kimataifa.

Baada ya kupoteza ngome yake ya mwisho ya Hajar al-Aswad na kambi yake ya Yarmouk katika mji wa Damascus Mei 22, kundi la Islamic State (IS) limeongeza mashambulizi yake dhidi ya jeshi la Syria na washirika wake.

OSDH inasema kuwa wapiganaji 180 wa makundi yanayounga mkono serikali waliuawa katika mashambulizi hayo. Askari wanne kutoka Urusi pia ni miongoni mwa waliouawa.

Wachanganuzi wa masuala ya usalama wanasema kundi la Islamic State bado lina nguvu kubwa katika jangwa la Badia, ambalo linaendelea hadi kwenye mpaka wa Iraq.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.