rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani Taliban

Imechapishwa • Imehaririwa

Askari 30 wa Afghanistan wauawa na Taliban

media
Majeshi ya Afghanistan yaendelea kupambana dhidi ya wapiganaji wa Taliban katika maeneo mbali ya nchi hiyo. REUTERS/Mohammad Ismail

Askari thelathini wa Afghanistan wameuawa Jumatano wiki hii katika shambulio la kuvizia la Taliban katika jimbo la Magharibi la Badghis, gavana wa jimbo hilo amesema.


Hili ni shambulio la kwanza kubwa la Taliban lililogharimu maisha ya askari wengi wa Afghanistan tangu kutangazwa kusitishwa mapigano kwa muda wa siku tatu, siku ya Jumapili, kutokana na sherehe za Eid el Fitr.

Majeshi ya Serikali pia yasitisha mapigano. Muda huo ungelimalizika leo Jumatano, lakini serikali ya Afghanistan ilikua iliongeza siku kumi.

Wapiganaji wa Taliban waliruhusiwa kushiriki mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe za kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhan katika miji kadhaa ya Afghanistan.