rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Syria Marekani Urusi

Imechapishwa • Imehaririwa

Wapiganaji zaidi ya 52 wa kigeni wauawa Syria

media
Wapiganaji wa Syrian Democratic Forces (SDF) na askari wa Marekani (kushoto), Mei 1, 2018 huko Boukamal, mkoa wa Deir Ezzor. AFP

Wapiganaji zaidi ya 40 wa kigeni wanaopigana upande wa serikali nchini Syria wameuawa katika mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za jeshi la serikali, mashariki mwa nchi hiyo, shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (SOHR) limesema Jumatatu wiki hii.


Kwa mujibu wa SOHR, mashambulizi hayo ya usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii, yaliua wapiganaji zaidi ya 25 yaliendeshwa na muungamo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani. Hata hivyo, shirika hili halijaweza kutambua chanzo cha mashambulizi hayo, ambayo yamesababisha hasara kubwa upande wa vikosi vya serikali.

"Wapiganaji thelathini na nane wasio kuwa raia wa Syria wanashirikiana na wanamgambo wanaounga mkono serikali ya Syria wameuawa katika mashambulizi ya usiku katika eneo la al-Hari, "amesema mkurugenzi wa SOHR, Rami Abdel Rahman.

Likinukuu chanzo cha kijeshi, shirika la habari la serikali, Sana, limesema kuwa watu kadhaa wameuawa na ndege za muungano unaoongozwa na Marekani.

Hata hivyo muungano huo havijatangaza kuwa vimetekeleza mashambulizi dhidi ya ngime za vikosi vya serikali nchini Syria.

Al Hari iko katika jimbo la mashariki la Deir Ezzor, tajiri kwa mafuta, ambapo wapiganaji wa Syrian Democratic Forces (SDF) wanaoungwa mkono na Marekani na vikosi vya Serikali ya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi wanaendelea na mashambulizi tofauti dhidi ya kundi la Islamic State ( IS).

Mnamo mwezi Mei, wengi wa wapiganaji wa serikali waliuawa katika masambulizi ya anga dhidi ya ngome za jeshi la Syria. OSDH na vyombo vya habari vya serikali ya Syria vilihusisha mashambulizi hayo muungano wa kimataifa unaoongizwa na Marekani, lakini Pentagon ilikanusha.