rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu zaidi 7 wauawa katika shambulizi dhidi ya viongozi wa dini Afghanistan

media
Mji muu wa Afghanistan, Kabul. REUTERS/Ahmad Masood/File Photo

Watu wasiopungua saba wameuawa na tisa wamejeruhiwa katika shambulizi la kujitoa muhanga lililotokea mjini Kabul Jumatatu wiki hii. Shambulizi ambalo lilinga mkusanyiko wa viongozi wa kidini ambao wamekua walitangaza msimamo wao dhidi ya ugaidi nchini humo.


Mshambuliaji, aliyekua akitembea kwa miguu, alijilipua mbele ya mlango wa hema ambapokulikua kukifanyika mkutano huo "loya jirga" ("mkusanyiko mkubwa" katika lugha ya Kipashto) uliojumuisha maelfu ya viongozi wa dini (Maulama) kutoka mikoa 34 ya Afghanistan. Shambulizi hili limeua na kujeruhi watu wa kawaida, kwa mujibu wa polisi walisema.

"Kwa mujibu wa taarifa zetu za kwanza, watu saba wameuawa, ikiwa ni pamoja na polisi mmoja, na watu wengine tisa wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na polisi wawili," msemaji wa polisi wa Kabul, Hashmat Stanikzai, ameliambia shirika la habari la AFP.

"Waathirika ni hasa wakazi wa mji huo, lakini kunaweza kuwa na wageni walioalikwa katika mkutano huo," msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Najib Danish, ameliambia shirika la habari la AFP, huku akithibitisha kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.

"Tumechukua hatua za usalama, lakini mshambuliaji alijifananisha mgeni atika mkutano huo, kabla ya kujilipua," ameongeza.

Viongozi wa dini walikua wakijianda kuondoka sehemu hiyo wakati shambulizi hilo lilitokea mapem amchana magharibi mwa mji mkuu wa Afghanistan.