Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-USALAMA

Hali ya utulivu yaanza kurejea Katika Ukanda wa Gaza

Hali ya utulivu imeanza kurejea katika Ukanda wa Gaza, baada ya makabiliano ya siku kadhaa kati ya wanajeshi wa Israeli na wapiganaji wa kundi la Hamas kutoka Palestina.

Ukanda wa Gaza ulikua ulikumbwa na mashambuloizi ya nege za kijeshi za Israel mapem awiki hii.
Ukanda wa Gaza ulikua ulikumbwa na mashambuloizi ya nege za kijeshi za Israel mapem awiki hii. REUTERS/Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Yamekuwa makabiliano mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu mwaka 2014.

Hamas imerusha mamia ya makombora katika ardhi ya Israeli huku jeshi la Israeli likisema limeshambulia ngime 65 za Hamas.

Israel inaeleza kuwa, makombora 70 kutoka upande wa Palestina yalirushwa siku ya Jumanne kuwalenga raia wa Israel.

Mengi ya maroketi hayo yalidunguliwa na mitambo hiyo ya Iron Dome, kwa mujibu wa jeshi.

“Mitambo ya kudungua makombora ya Israel maarufu kama "Iron Dome anti-missile shield", imedungua roketi zilizovurumisha kutoka Ukanda wa Gaza baada ya ving’ora kulia kusini mwa Israel kuwaonya raia kukimbilia maeneo salama, “ jeshi la Israel limesem akatika taarifa yake.

Siku ya Jumatatu wanajeshi wa Israel walimua mwanamgambo wa Hamas na kuwakamata wengine wawili waliojaribu kuvuka mpaka kwenda Israel.

Takriban wapalestina 116 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano na kuzua shutuma kali za kimataifa kutokana na mbinu ilizotumia Israel.

Israel inalaumu kundi la Hamas kwa kuchochea ghasia hizo, madai kundi hilo linakana.

Wasiwasi umeendelea kushuhudiwa kati ya Israel na Palestina, baada ya Marekani kuhamishia Ubalozi wake mjini Jerusalem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.