Pata taarifa kuu
MISRI-GAZA-USALAMA

Eneo la mpakani kati ya Gaza na Misri lafunguliwa

Rais wa Misri Abdel Fattah al Sissi ameagiza kufunguliwa kwa barabara ndogo ilio katika eneo la Rafah kati ya Ukanda wa Gaza na Misri katika kipindi chote hiki cha mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Wakazi wa Rafah awkijaribu kuingia nchini Misri kupitia barabara ndogo kati ya Ukanda wa Gaza na Misri iliyofunguliwa kwa agizo la Rais wa Misri Abdel Fattah al Sissi.
Wakazi wa Rafah awkijaribu kuingia nchini Misri kupitia barabara ndogo kati ya Ukanda wa Gaza na Misri iliyofunguliwa kwa agizo la Rais wa Misri Abdel Fattah al Sissi. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa
Matangazo ya kibiashara

Watu milioni mbili wanaoishi katika eneo hili la pwani wamekua wakisumbuliwa kuingia nchini Misri kupitia barabara hiyo kutokana na ukosefu wa usalama, ambapo utawala wa Misri uanendelea kukakabiliana na waasi wa Kiislamu. Misri ilifungua eneo hili la mpakani kwa muda manmo mwezi Februari mwaka huu.

Hii itasaidia "kupunguza mzigo kwa ndugu zetu huko Gaza," Rais al Sissi ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kando ya uzinduzi wa ubalozi mpya wa Marekani katika mji wa Jerusalem siku ya Jumatatu wiki hii, waandamanaji 52 wa Palestina, ikiwa ni pamoja na watoto sita, waliuawa na majeshi ya Israeli kwenye mpaka kati ya Ukanda wa Gaza na Israel, msemaji wa wizara ya afya ya Palestina ametangaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.