rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Israeli Palestina UNSC Nikki Haley

Imechapishwa • Imehaririwa

Machafuko Gaza: Marekani yatengwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

media
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. REUTERS/Eduardo Munoz

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana katika kikao chake cha dharura siku ya Jumanne wiki hii. Ilikua mara ya kwanza wanadiplomasia kujieleza hadharani tangu kuzuka kwa mashafuko katika ukanda wa Gaza Jumatatu wiki hii.


Machafuko hayo yalisababisha vifo vingi, tukio ambalo halijawahi kutokea katika eneo hilo tangu mwaka 2014.

Mkutano huo ulionyesha jinsi gani Marekani ilitengwa.

Mgawanyiko kati ya Marekani na Baraza la Usalama ulijitokeza kwa picha tatu: ile ya Nikki Haley, kwanza, balozi wa Marekani, alipoondoka mkutanoni wakati balozi wa Palestina kwenye baraza hilo Riyad Mansour kupewa nafasi ya kuzungumza. Na tukio la pili ni wakati mabalozi wa kundi kundi la nchi za Kiarabu kwenye Umoja wa Mataifa walipopiga picha wakimzunguka Balozi Mansour ambaye alikua akiomba ulinzi wa kimataifa kwa raia wake.

Dakika chache baadaye, mabalozi wa nchi za Ulaya walikuja na msimamo mmoja wakidaikusitishwa kwa vurugu hizo na kuitaka Israeli kujizuia katika matumizi ya nguvu, lakini pia Hamas kuachana na uchokozi.

Hata hivyo lawama hizi au shutma hizi zitabaki kuwa ni ishara tu kwani, Marekani ilizuia taarifa yoyote ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kama alivyokumbusha balozi wa Palestina: "Ni aibu kuona siku pekee kunatokea vifo vya Wapalestina 61 ikiwa ni pamoja na watoto 8 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaendelea kudhoofika. " Wapalestina, ambao wanomba ulinzi wa kimataifa, wanajua kuwa ombi lao halitashughulikiwa kwa sababu ya upinzani wa Washington.

Marekani imeonyesha wazi kuwa inaiunga mkono Israeli, ikisema kuwa Jerusalem ilikuwa mji mkuu wa serikali ya Wayahudi na kubaini kwamba hakutakuwa na makubaliano ya amani bila mji huo kutambuliwa kama mji mkuu wa Israeli.