rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Palestina Israeli Marekani

Imechapishwa • Imehaririwa

Hofu ya kutokea machafuko zaidi kati ya Israel na Palestina yatanda

media
Raia wa Palestina wakiandamana katika Ukanda wa Gaza, huku vikosi vya usalama na ulinzi vikitumia nguvu kupita kiasi kuzima maandamano, Mei 14, 2018. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa

Machafuko yaliyotokea Jumatatu, Mei 14, yaligharimu maisha ya watu 59 na zaidi ya 2,400 kujeruhiwa wakati majeshi ya Israeli yalitumia nguvu za kupita kiasi kuzima maandamano ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Hali hii haikuzuia Marekani kuendelea na sherehe ya uzinduzi wa ubalozi wake Jerusalem kama hatua ya kuelekea amani.


Jumanne wiki hii, Israeli inajiandaa kukabiliana na mgomo wa jumla katika maeneo ya Palestina na kuanza tena kwa maandamano ya siku ya Nakba, "janga" lililowasibu Wapalestina wakati taifa la Israeli lilitangazwa mwaka 1948.

Baada ya tukio baya kuwahi kutokea katika ukanda wa Gaza tangu operesheni iliyoitwa " Kinga ya ulinzi" katika majira ya joto ya mwaka 2014, amearifu mwandishi wa RFI Jerusalem, Michel Paul, Israeli inajiandaa kukabiliana na maandamano makubwa kwa siku ya Nakba ambayo inaadhimishwa Jumanne hii Mei 15. Vikosi vya usalama na ulinzi vimetumwa kwa wingi kando ya mpaka na Gaza. Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alifanya mazungumzo Jumatatu jioni na viongozi wa idara mbalimbali za usalama.

Israeli inalinda tu uhuru wake kama inavyofanya nchi nyingine yoyote, alisema Benjamin Netanyahu. Uamuzi wa Tsahal (IDF) umezuia Wapalestina kuingia katika eneo la Israeli, aliongeza. Chanzo cha kijeshi kimetishia kwamba ikiwa machafuko yataendelea kuongezeka Israeli itawalenga viongozi wa Hamas. Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi kutoka Israeli, Jumanne hii asubuhi barabara ndogo ya Kerem Hashalom ilio kati ya Israeli na Gaza itafunguliwa upya kwa amri ya Waziri wa Ulinzi wa Israel. Wakati huo huo Waisraeli wenye asili ya Kiarabu wanatarajia kuanza mgomo ili kulaani mauaji ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

"Siku kuu ya amani," alisema Benjamin Netanyahu katika uzinduzi wa ubalozi wa Marekani Jumatatu wiki hii mjini Jerusalemu.

Msemaji wa White House pia amezungumzia mpango wa amani ambao utawasilishwa na Marekani katika siku za usoni. Amesema, machafuko ya siku ya Jumatatu hayatakuwa na athari yoyote juu ya mafanikio ya mpango huu.