rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani Israeli Palestina

Imechapishwa • Imehaririwa

Wapalestina 45 wauawa katika makabiliano na jeshi la Israeli

media
Maandamano yenye vurugu yasababisha vifo vya watu 37 kwenye mpaka kati ya Gaza na Israel. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa

Waandamanaji arobaini na watano, raia wa Palestina, wameuawa katika mapigano na vikosi vya Israeli kwenye mpaka kati ya Ukanda wa Gaza na Israeli, mwandishi wa RFI ameripoti.


Watu 900 wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na 450 ambao wamepigwa risasi.

Hii ni idadi kubwa ya vifo kutokea kwenye mpaka wa Israel tangu kuanza kwa "Mandamano makubwa" ya Wapalestina manamo Machi 30 .

Maandamano haya yanatazamiwa kuendelea Jumanne, Mei 15, siku ambayo Wapalestina wanaita "Nakba" ( "janga"), ikimaanisha kufukuzwa kwa mamia ya maelfu ya Wapalestina wakati taifa la Israel lilipoundwa mnamo mwaka 1948.

Tangu mwishoni mwa mwezi Machi, waandamanaji 82 waliuawa na vikosi vya usalama vya Israel kwenye mpaka wa Gaza. Wakati huo hakuna raia wa Israel aliyeuawa.

Jeshi la Israel lilirusha vipeperushi katika Ukanda wa Gaza, na kuwataka wakazi wa eneo hilo "kutotumiwa" na kundi la Hamas, ambalo lina mamlaka katika Ukanda wa Gaza kwa zaidi ya miaka kumi, pia kuwataka kutothubutu kukaribia mpaka wa Israel na ukanda huo.