rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani

Imechapishwa • Imehaririwa

Milipuko mitatu yasikika katikati mwa mji wa Kabul

media
Afganistan yaendelea kukabiliwa na mdororo wa usalama. REUTERS/Omar Sobhani

Milipuko mitatu pamoja na milio ya risasi za rashasha imesikika Jumatano wiki hii katikati mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, kwa mujibu wa vyanzo vya polisi na Wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan.


Kwa mujibu wa mwakilishi wa wizara ya mambo ya ndani, shambulio la kujitoa mhanga limetekelezwa kwenye lango la kituo cha polisi katikati ya mji mkuu, katika karibu na majengo ya serikali na balozi mbalimbali.

"Tunatuma magari ya wagonjwa kwenye eneo la tukio na baadhi ya barabara zitafungwa," msemaji wa polisi amesema.

Haijafahamika ni watu wangapi ambao watakua wamepoteza maisha au kujeruhiwa na milipuko hiyo.

Watu 26, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari tisa waliuawa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyotokea Aprili 30 mjini Kabul.