Pata taarifa kuu
LEBANON-UCHAGUZI-SIASA

Raia wasusia uchaguzi Lebanon

Lebanon ilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa wabunge siku ya Jumapili Mei 6 baada ya karibu miaka kumi, kura ambayo iliitikiwa na watu wachache na huenda matokeo ya uchaguzi yakapelekea vyama vikuu mbalimbali kuagawana madaraka.

Kura zimeanza kuhesabiwa. Hapa ni katika kituo cha kupigia kura huko Beirut, Mei 6, 2018.
Kura zimeanza kuhesabiwa. Hapa ni katika kituo cha kupigia kura huko Beirut, Mei 6, 2018. REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kupigia kura vilifungwa saa moja usiku, saa za nch hiyo. Kwa jumla ya wapiga kura milioni 3.7, asilimia 49.2 pekee ndio walipiga kura, dhidi ya 54% mwaka 2009, Waziri Mambo ya Ndani, Nohad Machnouk, alisema jana jioni.

Raia walisusia uchaguzi huo wakati ambapo sheria mpya ya uchaguzi inayohusu uwiano iliyopitishwa mwaka jana na kwamba wapiga kura wapya wapatao 800,000 walipaswa kupiga kura. "Sheria hii ilitarajiwa kuwa ingelipelekea kiwango cha ushiriki kuwa juu zaidi kuliko mwaka 2009," alisema Machnouk.

Lakini "wapiga kura na viongozi wa vituao vya kupigia kura bado hawajazoea sheria hii mpya, hali ambayo imesababisha kupungua kwa kasi mchakato wa kupiga kura," aliongeza.

Zoezi la kuhesabu kura ilianza mapema jioni lakini matokeo ya mwisho yanatarajiwa kujulikana kabla ya Jumatatu wiki hii.

Kwa mujibu wa wataalamu, matokeo ya uchaguzi hayapaswi kushangaza wengi, na bunge, lenye wajumbe 128, litatawaliwa na vyama vya jadi, ikiwa ni pamoja na chama kikuu cha Hezbollah, mshirika wa Syria na Iran.

"Hezbollah ina nafasi kubwa ya kuwa na ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi lakini itategemea ushirikiano wake na vyama vingine" mchambuzi wa kisiasa, Karim el-Mufti, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kwa upande wa Waziri Mkuu kutoka dhehebu la Sunni, Saad Hariri, anayeungwa mkono na Saudi Arabia, chama chake cha kisiasa "kinaweza kupoteza viti vichache, lakini nafasi yake haikabiliwi na tishio lolote," ameongeza mchambuzi huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.