Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA-HAKI

Syria kutolewa msaada wa kibinadamu

Wafadhili wa Kimataifa wanatarajiwa kukutana leo jijini Brussels nchini Ubelgiji, kuahidi Mabilioni ya Dola kusaidia katika utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Syria.

Hali ya kibinadamu inatisha Syria, huku mapigano yakitokea kila kukicha.
Hali ya kibinadamu inatisha Syria, huku mapigano yakitokea kila kukicha. AFP/Syrian Governement's Central Military Media
Matangazo ya kibiashara

Hali inaendelea kuwa mbaya nchini humo hasa katika jimbo la Idlib.

Umoja wa Mataifa unasema unahitaji angalau Dola Bilioni 8 kuwasaidia raia hao wa Syria, wanaoishi ndani na nje ya nchi hiyo.

Umoja wa Mataifa na mashirika ya wahisani yamekuwa yakipiga kelele juu ya kupatikana kwa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kuwatolea msaada wa kibinadamu waathirika wa vita hivyo vilivyo gharimu hadi sasa maisha ya watu laki moja na elfu thelathini na wengine milioni 2.4 wakikimbia makwao.

Hii sio mara ya kwanza wafadhili wa kimataifa kukutana kwa ajili ya kuitolea Syria msaada wa kibinadamu.

Mnamo mwaka 2016,wafadhili na marafafiki wa Syria walikutana nchini Kuwait na kuahidi kutoa ahadi ya dola bilioni 2 nukta 4 kusaidia hali ya Kibinadamu nchini humo kutokana na machafuko yanayoendelea. Wajumbe kutoka Mataifa Sabini duniani na Mashirika 24 ya Kimataufa walikuatana chini ya uongozi wa katibu mkuu Ban Ki Moon ambaye alisema ahadi iliyotolewa haikufikia nusu ya fedha zinazohitajika ambazo ni zaidi ya dola Bilioni 6 kuwasaidia raia wa syria wanaoishi katika mazingira magumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.