rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Mashambulizi ya bomu yaua watu 63 Kabul

media
Timu ya wachunguzi ikifanya uchunguzi katika eneo la shambulio katika kituo cha kujiandikisha Kabul, Aprili 22, 2018. REUTERS/Omar Sobhani

Watu 63 wamepoteza maisha jijini Kabul nchini Afghanistan baada ya kutokea kwa mashambulizi ya bomu katika maeneo mbalimbali ya kujiandikisjha kama wapiga kura.


Taarifa kutoka mamlaka mjini Kabul zinasema kuwa wanawake 21 na watoto watano ni miongoni mwa waliouawa, kwa mujibu wa mashahidi. Watu 119 wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Mlipuko huo pamoja na kusababisha vifo lakini pia umeharibu magari magari.Hadi sasa kumekuwa na mashambulio manne tangu kuanza uandikishaji huo wiki iliyopita.

Kundi la Islamic State limesema ndilo lililohusika na shambulizi hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kazi ya uandikishaji wapiga kura nchini humo imeanza mwezi uliopita ikiwa ni maandalizi kwaajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Ripoti zinasema kuwa, idadi kubwa ya watu walipoteza maisha ni wanawake na watoto.