rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Syria UN UNSC Haki za Binadamu

Imechapishwa • Imehaririwa

Syria yakabiliwa na madai ya shambulizi la kemikali

media
Katika hospitali Aprili 7 huko Duma, baada ya madai ya mashambulizi ya kemikali. White Helmets/Reuters TV via REUTERS

Watalaam wa silaha za kemikali wanatarajiwa kuwasili mjini Douma nchini Syria kesho kuanza kazi ya kuchunguza iwapo silaha hizo zilitumiwa kuwashambulia raia wasiokuwa na hatua wiki mbili zilizopita.


Ripoti ya kuwasili kwa watalaam hao, imetolewa na maafisa wa Urusi wakati huu Marekani ikisema inahofia kuwa tayari Moscow imeharibu ushahidi kabla ya watalaam hao kufika.

Nchini Uingereza, Waziri Mkuu Theresa May naye amewaelezea wabunge ni kwanini jeshi la nchi hiyo, liliamua kuungana na lile la Marekani na Ufaransa kushambulia maeneo yanayoaminiwa kuwa na silaha za kemikali huko Syria.

Wabunge walikuwa wamehoji ni kwanini Waziri Mkuu May aliamua kushambulia Syria bila ya idhini yao.

Siku ya Jumamosi wili iliyopita, nchi za Marekani, Ufaransa na Uingereza ziliendesha mashambulizi katika maeneo muhimu yanayoaminiwa kuwa zinafichwa silaha za kemikali nchini Syria. Mashambulizi hayo yalikuja wiki moja baada ya serikali ya Syria kufanya mashambulizi katika mji wa Duma, mashambulizi ambayo nchi za magharibi zilidai kua silaha za kemikali zilitumiwa.