rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani Taliban

Imechapishwa • Imehaririwa

Zaidi ya watu 100 wauawa katika chuo Afghanistan

media
Mmoja wa watu waliojeruhiwa katika shambulio la ndege ya jeshi la Afghanistan katika hospitali ya Kunduz Aprili 2, 2018. AFP

Zaidi ya watu 100, ikiwa ni pamoja na watoto wengi, wameuawa na wengine kujeruhiwa jana Jumatatu katika shambulizi la bomu lililotekelezwa na ndege ya jeshi la Afghanistan.


Shambulio hilo lilitokea katika chuo cha dini (madrasa) kaskazini mashariki mwa Afghanistan, kulingana na ripoti kutoka hospitali na vyanzo vya usalama.

Siku moja baada ya shambulio hilo, vyanzo viwili vya usalama ambavyo havikutaka kutajwa majina yao vilmeeleza kwamba shambulio hilo liligharimu maisha ya watu "59 , wengi wao ikiwa ni watotowalio a umri kati ya 8 na 17 "pamoja na" watu 57 waliojeruhiwa ".

Shambulio hilo lilitokea Jumatatu mchana wakati wa sherehe ya kuhitimu visomo mwaka katika chuo hicho cha dini (madrasa), katika wilaya inayodhibitiwa kwa kiasi kikubwa na kundi la Taliban.

Msemaji wa Wizara ya Afya mjini Kabul, Wahid Majroh, amethibitisha leo Jumanne asubuhi kuwa "watu 57, ikiwa ni pamoja na watoto na wazee, walisafirishwa hospitalini katika mkoa wa Kunduz na watano waliopoteza maisha."

Chanzo cha usalama kinasema kuwa wapiganaji wa Taliban "huwa hawawapeleki waathirika wao katika hospitali za umma".

Shahidi mmoja ambaye aliwasili katika eneo hilo baada ya shambulio hilo, Abdul Khalil, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "amehesabu miili 35, wengi wao walipoteza viongo vyao vya mwili".