Pata taarifa kuu
GAZA-ISRAEL-PALESTINA

Palestina: Raia 7 wauawa na vikosi vya Israel Gaza

Raia 7 wa Palestina wameuawa na vikosi vya Israel kwenye eneo la ukanda wa Gaza wakati huu kukishuhudiwa makabiliano makali kwenye eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.

Waandamanaji wa Kipalestina wakirusha mawe kuelekeza kwa askari wa Israel, Machi 30, 2018.
Waandamanaji wa Kipalestina wakirusha mawe kuelekeza kwa askari wa Israel, Machi 30, 2018. REUTERS/Ibraheem Abu Mustafa
Matangazo ya kibiashara

Mahmoud Rahmi amekuwa raia wa 7 kuuawa baada ya kupigwa risasi wakati akiwa mstari wa mbele kukabiliana na askari wa Israel, haya yakiripotiwa kuwa makabiliano mabaya zaidi katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Kifo chake kimeripotiwa baada ya raia mwinhine Jihad Farina na Ahmed Ouda kuuawa kwa kupigwa risasi, imesema taarifa ya wizara ya afya.

Waandamanaji wengine watatu walipigwa risasi kwenye maandamano wakati mkulima mmoja aliuawa kwa kupigwa na roketi akiwa shambani kwake.

Maelfu ya waandamanaji wa Kipalestina walijitokeza kwenye mpaka wa nchi hiyo na Israel, maandamano ambayo awali kundi la Hamas linalokalia eneo hilo lilidai yatakuwa ya amani.

Kundi la waandamanaji wachache walijaribu kusogea kwenye eneo la mpaka lenye ulinzi mkali kwa lengo la kuangusha waya uliowekwa kuwazuia kabla ya wanajeshi wa Israel kutumia risasi za moto kuwatawanya.

Jeshi la Israel limesema kuwa waandamanaji walikuwa wakiwarushia mawe na mabomu ya kutengeneza kwa mkono hatua iliyowalazimu wanajeshi wake kujibu kwa risasi za moto.

Shirika la msalaba mwekundu la Palestina limedai kuwa jumla ya watu 200 walihudumiwa kwa majeraha ya risasi za moto.

Maandamano haya yamefanyika katika maadhimisho ya siku ya Ardhi ambayo ni kumbukumbu ya Machi 30, 1976 wakati raia 6 wa Kipalestina waliuawa na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano ya kupinga nchi hiyo kuchukua ardhi yao kwa nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.