Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-UPINZANI

Upinzani nchini Syria yasema UN imeshindwa kumaliza vita Ghouta Mashariki

Kiongozi wa wapiganaji wa upinzani nchini Syria, ameulaumu Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuzuia mauaji ya raia Mashariki mwa Ghouta.

Ngome ya upinzani Mashariki mwa Ghouta baada ya vita kusababisha watu kukimbia makwao
Ngome ya upinzani Mashariki mwa Ghouta baada ya vita kusababisha watu kukimbia makwao ABDULMONAM EASSA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nasr al-Hariri, ambaye amekuwa akiongoza ujumbe wa upinzani wakati wa mazungumzo ya amani, amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaa kimya wakati raia wanapoendelea kushambuliwa na kuuawa.

Aidha, ameishtumu serikali ya rais Bashar al Assad na serikali ya Urusi kwa kuendelea kuwalenga raia wasiokuwa na hatia na kusema ni lazima siku moja waajibishwe.

Kauli hii ya upinzani inakuja wakati, huu jeshi la Syria likiwa limechukua asilimia 70 ya ngome hiyo ya mwisho ya upinzani.

Watu 1,400 wengi wao wakiwa raia wa kawaida wameuawa katika vita Ghouta Mashariki ndani ya miezi miwili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.