Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-VITA

UN, Marekani zachoshwa na vita nchini Syria

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa nchi wanachama za baraza la usalama kumaliza mahambulizi yanayoendelea kushuhudiwa Mashariki mwa mji wa Ghouta nchini Syria.

Athari ya mashambulizi katika ngime ya upinzani Mashariki mwa Ghouta
Athari ya mashambulizi katika ngime ya upinzani Mashariki mwa Ghouta REUTERS/Bassam Khabieh.
Matangazo ya kibiashara

Wakati uo huo, Marekani imetishia kuchukua hatua ikiwa usitishwaji wa mapigano kama ambavyo iliamuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utaendelea kudharauliwa na Serikali ya Syria na Urusi.

Balozi wa Marekani kwenye umoja wa Mataifa Nikki Halley amesema nchi yake haitaendelea kuvumilia kuona wananchi wa mji wa Ghouta wakiendelea kutaabika kutokana na mashambulizi yanayoendeshwa na vikosi vya Serikali na washirika wake.

Majaribio kadhaa ya kusitisha mashambulizi kwenye huo yameshindikana huku mpaka sasa watu zaidi ya elfu 1 wakiripotiwa kuuawa katika mashambulizi yanayofanywa na Urusi na vikosi vya Serikali ya Syria kwenye mji huo kwa muda wa wiki nne zilizopita.

Siku ya Jumatatu, waangalizi wa mzozo huu walitoa takwimu zinazoonesha kuwa watu zaidi ya 350,000 wameuawa kutokana na vita vinavyeondelea, vinavyoingia mwaka wa nane siku ya Alhamisi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.