rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Syria UNSC Urusi

Imechapishwa • Imehaririwa

Idadi ya watu waliopoteza maisha Mashariki mwa Ghouta yafika 800

media
KIkao kilichopita cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa REUTERS/Eduardo Munozrs

Mashambulizi ya jeshi la Syria katika ngome ya upinzani Mashariki mwa Ghouta, yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 800, kwa mujibu wa waangalizi wa mzozo huu.


Miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni watoto 178, tangu kuanza kwa operesheni hiyo tarehe 18 mwezi Februari.

Takwimu hizi zimetolewa wakati huu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kukutana kujadili mzozo huu hasa hatua ya Syria kukataa kusitisha vita kwa siku 30 kama ilivyoagizwa.

Urusi ambayo inaisaidia Syria, siku ya Jumanne ilipoteza raia wake 39 baada ya ndege ya abiria kuanguka katika kambi ya kijeshi nchini Syria.

Kuendelea kwa vita, kumesababisha mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu kutowafikia waathiriwa.

Mapema wiki hii, rais Bashar Al Assad alisema mapigano katika ngome hiyo ya upinzani inayosalia jijini Damascus, yataendelea hadi pale wapinza wake watakaposhindwa.