Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-UGAIDI

Malori ya misaada ya kibinadamu yanakwenda Mashariki mwa Ghouta

Malori iliyobeba misaada ya kibinadamu ipo njiani kwenda katika ngome ya upinzani Mashariki mwa Ghouta viungani mwa jiji la Damascus nchini Syria.

Rais wa Syria Bashar Al Assad
Rais wa Syria Bashar Al Assad HO / SANA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Kimataifa la Msalaba mwekundu limesema hatimaye misaada ya kibinadamu inakwenda kuwasaidia maelfu ya raia wasiokuwa na hatia ambao wamekwama katika eneo hilo la vita.

Malori 46 kutoka kwa Shirika la Kimataifa la msalaba mwekundi, pamoja na lile la Syria na kutoka Umoja wa Mataifa yamebeba chakula, dawa na mahitaji muhimu.

Wakati uo huo, rais wa Syria Bashar amesema wanajeshi wake wataendelea kushambulia ngome ya wapinzani Mashariki mwa Ghouta, licha ya wito wa kusitishwa kwa vita.

Kauli hii ya Assad imekuja wakati huu jeshi la Syria linalosaidiwa na lile la Urusi likiendelea kuwashambulia wapiganaji wa upinzani, huku vifo vya watu 34 vikiripotiwa mwishoni mwa wiki lililopita pekee.

Makabiliano hayo katika ngome hiyo ya upinzani inayosalia jijini Damascus kwa kipindi cha wiki nne zilizopita, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 600 wasiokuwa na hatia.

Waangalizi wa mzozo huu wanasema, tayari wanajeshi wa Syria wamefanikiwa kudhibiti asilimia 10 ya ngome hiyo ya upinzani.

Marekani, Ufaransa na Uingereza yameishtumu serikali ya Syria kwa kuendeleza vita licha ya kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa, kutaka vita kukomeshwa kwa siku thelathini kuwaruhusu maelfu ya waathiriwa kupata misaada ya kibinadamu.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.