Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-SIASA-USALAMA

Mfalme Salman amfuta kazi mkuu wa majeshi Saudi Arabia

Utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia umechukua uamuzi wa kuwafuta kazi maafisa wa vyeo vya juu jeshini akiwemo mkuu wa majeshi.

Mfalme Salman, Riyadh mnamo Februari 26, 2018, alitoa mfululizo wa maagizo yanayowafuta kazi maafisa kadhaa wa ngazi za juu katika jeshi la Saudi Arabia.
Mfalme Salman, Riyadh mnamo Februari 26, 2018, alitoa mfululizo wa maagizo yanayowafuta kazi maafisa kadhaa wa ngazi za juu katika jeshi la Saudi Arabia. REUTERS/Faisal Al Nasser
Matangazo ya kibiashara

Baada ya sakata dhidi ya rushwa mwishoni mwa mwaka jana katika sekta mbalimbali nchini Saudi Arabia na katika familia ya kifalme, muda umewadi sasa kukabiliana na kashfa hiyo katika jeshi.

Mfalme Salman ametoa mfululizo wa maagizo ambapo Mkuu wa majeshi na maafisa wengine wa ngazi za juu katika jeshi wamefutwa kazi na nafasi zao kuchukuliwa na maafisa wengine walioteuliwa.

Mfululizo wa maagizo ya kifalme yoliyotolewa jana Jumatatu usiku, Februari 26 yamelenga wizara ya ulinzi, inayoongozwa na Mwanamfalme mrithi Mohammed bin Salman.

Hakuna maelezo rasmi yaliyotolewa kuhusu mabadiliko hayo, lakini mabadiliko hayo yanakuja wakati ambapo vita vya Yemen vinaendelea kupamba moto. Uongozi wa majeshi nchini Saudi umefanyiwa mabadiliko makubwa. Mkuu wa majeshi, Jenerali Abdel Rahman bin Saleh al-Bunyan amefutwa kazi, na kuteuliwa kuwa mshauri katika mahakama ya kifalme. Nafasi yake imechukuliwa na Luteni Jenerali Fayyad al-Ruwaili. Wakuu wa vikosi vya angani na nchi kavu pia wametimuliwa kwenye nafasi zao.

Nafasi ya Naibu Waziri iapewa mwanamke

Maagizo ya kifalme yanatangaza mfululizo wa uteuzi mpya katika wizara nyingine kadhaa. Nafasi ya Naibu Waziri wa Kazi imeapewa mwanamke, Tamadur Bint Youssef al-Ramah.

Mfalme wa Saudi Salman ben Abdelaziz al-Saud pia ameamua kuteua Manaibu watatu wa wakuu wa mikoa kati ya watoto wa ndugu zake, Princes Ahmed, Talal na Muqrin, ambao baadhi yao wamekua wakisema kuwa wametengwa.

Gavana mpya wa mkoa wa Asir ni Mwanamfalme Turki bin Talal, nduguye Billionea Al Walid bin Talal, aliyekamatwa mnamo mwezi Novemba na kufungwa kwa muda wa miezi miwili katika hoteli ya kifahari ya Ritz Carlton mjini Riyadh na wakuu wengine kadhaa na viongozi waandamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.