Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-USALAMA

Guterres atoa wito wa kusitisha mapigano Syria

Katibu Mkuu wawa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kusitisha mara moja mapigano kwa muda wa siku 30, hatua iliyopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mbele ya Tume ya haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mbele ya Tume ya haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa. AFP
Matangazo ya kibiashara

WAkati huo huo Umoja wa Ulaya umezitaka pande zinazohasimiana kusitisha mapigano ili kuruhusu misaada kwa raia wa eneo hilo wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na dawa.

Hayo yanajiri wakati ambapo mashambulizi ya anaga yameendelea leo Jumatatu katika eneo la Ghouta mashariki linaloshikiliwa na waasi, huku likizingirwa na majeshi ya serikali na yale ya Urusi.

"Nakaribisha hatua ya kupitishwa kwa azimio hili na Baraza la Usalam la Umoja wa Mataifa, lakini nasubiri azimio hilo kuanza liweze kutekelezwa mara moja ili misaada na huduma za kibinadamu viweze kuwafikia mara moja walengwa, kuondoa wagonjwa walio katika hali mbaya na majeruhi, ili kupunguza mateso kwa raia wa Syria, "Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametangaza mbele ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

"Jitihada za kukabiliana dhidi ya ugaidi hazipewi kipaumbele," Bw Guterres amesema, wakati ambapo Iran, mshirika mkubwa wa serikali ya Syria, ilisema jana Jumapili kuwa mashambulizi dhidi ya "makundi ya kigaidi" yataendelea. katika eneo la Ghouta, ngome ya waasi.

Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein, amesema ni muhimu "kuwa makini"kuhusu ya hali inayoendelea Syria "kwa sababu mashambulizi ya angani yanaendelea".

Pia amelaani "mauaji ya dgidi ya binadamu" nchini Syria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Yemen na Burma.

Zeid Ra'ad Al Hussein ameshutumu wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "kuhusika" na muendelezo huo wa mateso makubwa kwa raia," kwa kutumia kura ya turufu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.