Pata taarifa kuu
SYRIA-MAUAJI-USALAMA

Watu 33 wauawa katika mashambulizi ya angani Idlib, Syria

Mashambulizi ya angani katika maeneo ya waasi katika mkoa wa Idlib, kaskazini-magharibi mwa Syria yamegharimu maisha ya watu wasiopungua 33 tangu Jumapili, maafisa wa uokoaji wa shirika la haki za binadamu nchini Syria,OSDH, wamearifu.

Wakaazi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Idlib wameyatoroka makazi yao kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi.
Wakaazi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Idlib wameyatoroka makazi yao kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi. REUTERS/Ammar Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Wengi wa waathirika waliorodheshwa katika mji wa Saraqib, kwenye barabara inayoelekea Aleppo, kilomita 20 kaskazini magharibi mwa kambi jeshi la anga iliyodhibitiwa hivi karibuni na vikosi vya serikali vya Syria na washirika wao.

Mashambulizi ya angani ya jeshi la Syria katika mkoa wa Idleb yameua watu wasiopungua 33 katika masaa 24 yaliyopita.

Siku ya Jumatatu pekee, mashambulizi hayo yaliua watu 16, ikiwa ni pamoja na watu 11 waliokuwa katika soko la jiji la Saraqeb, OSDH imesema.

Jumapili pekee, watu 17 waliuawa katika mashambulizi ya angani, mashambulizi ambayo yalilenga maeneo kadhaa ya Idleb, kwa mujibu wa mkurugenzi wa OSDH, Rami Abdel Rahman.

"Ndege za kivita za serikali ya Syria zimeongeza mashambulizi yake katika masaa 24 yaliyopita, baada ya utulivu kuliyotokana na hali mbaya ya hewa," amesema.

Majeshi ya nayounga mkono serikali ya Syria yakisaidiwa na mshirika wao Urusi yalizindua operesheni kabambe tarehe 25 Desemba ili kurejesha kwenye himaya yao eneo la kusini mashariki mwa Idleb, ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa kijeshi wa Abu Douhour.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.