Pata taarifa kuu
PALESTINA-MAREKANi-USHIRIKIANO-UCHUMI

Palestina: vitisho vya Donald Trump havina nafasi

Uongozi wa Mamlaka ya Palestina umelaani vitisho vya rais wa Marekani Donald Trump kuwa nchi hiyo itasitisha misaada yote iwapo itakataa kuzungumza na Israel kwa lengo la kutatua mzozo wa muda mrefu na kujaribu kupata amani ya kudumu.

RAis wa Mamlaka ya Mahmoud Abbasalaani vitisho vya rais Donald Trump.
RAis wa Mamlaka ya Mahmoud Abbasalaani vitisho vya rais Donald Trump. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa rais Mahmod Abaas, Nabil Abu Rudaineh, amesema vitisho hivyo havitatisha Wapalestina.

Trump ametoa viticho hivyo baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pemenzoni mwa mkutano wa uchumi mjini Davos nchini Uswizi.

Akizungumza katika kongamano la kiuchumi mjini Davos, Switzerland, bwana Trump alisema kuwa Marekani inawapatia Palestina mamia ya mamilioni ya madola kama msaada na usaidizi kila mwaka.

Wizara ya mashauriano ya kigeni ya Marekani imethibitisha kuwa Donald trump alikuwa akizungumzia msaada wa kiuchumi na usaidizi wa kiusalama.

Bwana Trump aliishutumu Palestina kwa kuivunjia heshima Marekani akisema ''kwa nini tuwafanyie kitu na wao wenyewe hawatufanyii chochote''.

Alilalamikia hatua ya uongozi wa Palestina wa kukataa kukutana na makamu wa rais wa Marekani Mike Pence katika eneo hilo mapema wiki hii.

Palestina imeikataa Marekani kuwa mpatanishi asiyependelea upande wowote katika mazungumzo hayo ya amani.

Mmalaka ya Palestina imekasirishwa na hatua ya Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.