rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu wasiopungua 40 waangamia Afghanistan

media
Hoteli Intercontinental, Kabul mnamo Januari 21, 2018 baada ya shambulizi la Taliban lililoua watu zaidi ya 40. REUTERS/Omar Sobhani

Watu zaidi ya 40 waliuawa katika shambulio la hoteli ya Intercontinental mjini Kabul mwisho wa wiki iliyopita, ikiwa ni pamoja na raia 25 kutoka Afghanistan na wageni 15, kulingana na vyanzo vya Afghanistan na kidiplomasia.


"Ripoti ya mwisho inasema watu 25 kutoka Afghanistan waliuawa katika shambulio la hoteli Intercontinental," msemaji wa wizara ya Afya, Wahid Majrooh, ameliambia shirika la habari la AFP leo Alhamisi, akiongeza kuwa raia wa kigeni 15 wamethibitishwa na balozi zao na serikali zao. Raia wanne kutoka Marekani ni miongoni mwao, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitangaza jana Jumatano jioni.

"Hatujishughulishi na majeruhi wa kigeni," amesema Majrooh, akiongeza kuwa waliojeruhiwa raia 12 wa Afghanistan pia walipokelewa katika hospitali za serikali zinazosimamiwa na wizara hiyo.

Wageni, waliokufa au kujeruhiwa, walipelekwa kwenye hospitali ya kijeshi ya Kabul au ile ya NDS, idara ya ujasusi ya Afghanistan.

Kwa jumla, raia kutoka mataifa kumi na sita tofauti walikuwepo jioni ya siku ya shambulio la hoteli Intercontinental (inayomilikiwa na serikali ya Afghanistan), ambayo tayari ilishambuliwa mwaka 2011 , kulingana na chanzo cha usalama.