rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Syria

Imechapishwa • Imehaririwa

Syria yashtumiwa kutekeleza mashambulizi mapya ya kemikali

media
Mvulana mdogo wa Syria akitumia chupa la oksijeni kwa mtoto katika hospitali ya Duma, Ghouta mashariki, mashariki mwa Damescus, baada ya mashambulizi ya kemikali, Januari 22, 2018. AFP

Watu wasiopungua 21, ikiwa ni pamoja na watoto, wameripotiwa kukosa hewa leo Jumatatu nchini Syria katika mji wa Ghouta mashariki, eneo linaloshikiliwa na waasi wanaoendelea kuzingira mashariki mwa Damascus.


Shirika la Haki za Binadamu nchini humo la OSDH limeshtumu utawala wa Syria kuendesha mashambulizi mapya ya kemikali.

Watu tisa pia wameuawa baad ya waasi kurusha mabomu katika kati moja ya mji wa Damascus, kulingana na televisheni ya serikali ya Syria.

Tangu kuanza kwa vita nchini Syria mnamo mwaka 2011,utawala wa Bashar al-Assad umeshtumiwa mara kadhaa na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kutumia gesi ya klorini au gesi ya sarin katika mashambulizi ya kemikali wakati mwingine yalisababisha vifo.

"Baada ya roketi kurushwa na vikosi vya serikali katika eneo la magharibi mwa mji wa Douma, mosi mweupe ulisambaa, na kusababisha watu 2 kukosa hewa," shirika la Haki za Binadamu la Syria OSDH limetangaza.

Katika hospitali ya Duma, watoto wachanga waliofunikwa na mablanketi, waliokua wakibebwa na ndugu au wazazi wao, wameonekana wakipumua kwa kutumia chupa la oksijeni, na baadhi wakitokwa na machozi, mwandishi wa shirika la habari la AFP amesema.

Watoto sita na wanawake sita ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa, kwa mujibu wa OSDH.