Pata taarifa kuu
UTURUKI-SYRIA-KURDI

Uturuki yashambulia ngome za wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria

Uturuki imezindua mashambulizi ya angaa na ya ardhini dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi Kaskazini ma Syria, licha ya onyo kutoka kwa Marekani.

Wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria
Wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria REUTERS/Rodi Said/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Marekani ambayo imewapa silaha wapiganaji hao kusaidia katika vita dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria, inasema kuwashambulia wapiganaji hao, kutahatarisha zaidi usalama wa Syria.

Hatua hii imekuja baada ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kusema kserikali yake inawatambua wapiganaji hao wa Kikurdi kama magaidi na maadui wa nchi yake.

Tayari ndege za kivita za Uturuki, zimeshambulia maeneo 108 za Kikurdi ikiwemo kambi yao Kaskazini mwa mji wa Allepo.

Ankara inasema ndege zake 72, zilihusika katika shambulizi hilo na kurejea salama katika kambi zao.

Aidha, Uturuki inasema kuwa kambi za Islamic State zimeharibiwa katika shambulizi hilo.

Pamoja na hilo, Uturuki inasema iliiambia Syria kuhusu operesheni hiyo lakini serikali ya Damascus imesema haikuambiwa lolote.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.