rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uturuki Syria Recep Tayyip Erdogan

Imechapishwa • Imehaririwa

Uturuki yatuma askari wengi kwenye mpaka na Syria

media
Askari 30,000 wanatarajiwa kupiga kambi kwenye mpaka na Syria. DOGAN NEWS AGENCY / AFP

Uturuki imetuma wanajeshi zaidi katika mpaka wake na Syria, baada ya Marekani kupendeza kuwepo kwa kikosi cha wanajeshi 30,000 kulinda usalama Kaskazini Mashariki mwa Syria.


Syria na Urusi pia zimepinga mpango huo wa Marekani, kwa kile wanachosema uwepo wa kikosi hicho, utasababisha kudorora zaidi kwa usalama nchini humo na kuunda makundi zaidi ya waasi.

Marekani inasema kikosi hicho kikishirikiana na wapiganaji wa Kikurdi kitasaidia kupambana na magaidi wa kundi la Islamic State Kaskazini Mashariki mwa Syria.

Syria imeendelea kukumbwa na mapigano kati ya waasi wakisaidiwa na Marekani na washirika wake upande mmoja na serikali ikisaidiwa na Urusi upande mwengine.

Urusi na Uturuki wamekua wakishtumu Marekani na mshirik wake mkuu katika vita hivyo Saudi Arabia kuwasaidia wapiganaji wa kundi la Islamic State, madai ambayo Marekani imefutilia mbali na kuilaumu Urusi kuendelea kuchochea vita nchini Syria.