rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Israeli Palestina

Imechapishwa • Imehaririwa

Israel yaidhinisha ujenzi wa nyumba 1,100 Ukingo wa Magharibi

media
Jeshi la Israeli katika eneo la shambulizi katika Ukingo wa Magharibi, Novemba 22, 2015. REUTERS/Ronen Zvulun

Mamlaka nchini Israel zimeidhinisha ujenzi wa makazi mapya ya walowezi zaidi ya elfu moja na mia moja kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi, hatua inayozidi kupandisha joto la mvutano kati ya nchi hiyo na Palestina.


Uidhinishwaji wa ujenzi wa makazi haya ulitangazwa hapo jana na tume ya wizara ya ulinzi, hatua inayokuja wakati huu Marekani ikiwa tayari imetangaza kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem kutoka Tel-Aviv.

Shirika lisilo la kiserikali linalopigania amani , limesema makazi mapya 352 tayari yamepata kibali cha kuanza ujenzi huku mengine yakiwa kwenye mchakato wa awali kuidhinishwa.

Kwa mujibu wa shirika hilo jumla ya nyumba elfu 6742 ziliidhinishwa kujengwa kwenye mradi wa mwaka jana peke yake ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu mwaka 2013.

Hivi karibuni Marekani ilichukua hatua ya kutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, hatua ambayo ilizua maandamano ya hasira katika nchi za Kiarabu.

Hatua ya Marekani ilifutiliwa mbali na Umoja wa Mataifa.