rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Israeli Palestina Benjamin Netanyahu

Imechapishwa • Imehaririwa

Netanyahu ataka kufungwa kwa shirika linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina

media
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. @reuteurs

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netayahu ametaka kufungwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi wa Kipalestina.


Wito huu wa Netanyahu umekuja baada ya Marekani kutishia kusitisha msaada wa kifedha kwa mamlaka ya Palestina.

Israel imekuwa ikisema kuwa Shirika hilo limekuwa likiendeleza shughuli zake kwa ubaguzi na kuwasajili Wapalestina wasiokuwa na vigezo kuwa wakimbizi.

Hivi karibuni Marekani imechukua hatua ya kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, uamuzi uliopingwa na Umoja wa Mataifa na jumuiya ya nchi za Kiislamu ambayo ilitangaza kuwa inatambua Jerusalem ya Mashariki kama mji mkuu wa Palestina.

Uamuzi huo wa Marekani umesababisha kuzuka kwa maandamano katika nchi mbalimbali, hasa zile za Kiarabu na katika maeneo mbalimbali ya Palestina. Watu kadhaa wamekamatwa na polisi wa Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi.