rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Palestina Israeli Marekani

Imechapishwa • Imehaririwa

Palestina yamuita balozi wake kutoka Marekani

media
Kiongozi wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas akosoa vikali hatua ya Marekani juu ya Israel. REUTERS/Eduardo Munoz

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amechukua uamuzi wa kumuita baloze wa nchi hiyo kutoka Marekani akisema Marekani haina nia nzuri na nchi yake na kufuatia hatua ya Donald Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.


Hatua ya Marekani ya Kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, imeendelea kuzua hali ya sintofahamu katika miji mbalimbali ya Palestina, huku maandamano yakiendelea katika nchi za Kiarabu.

Hivi karibuni jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiislam ilitangaza kutambua Jerusalem mashariki kama mji mkuu wa Palestina na kufutilia mbalimbali hatua ya Marekani ya kutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.

Azimio la Umoja wa Mataifa la hivi karibuni la kuitaka Marekani kufuta tangazo hilo lake liliunga mkono kwa wingi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Siku ya Jumapili Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas aliutaja mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa kiroho wa watu wa Palestina.

Israel ilitwaa eneo la mashariki mwa mji, ambalo awali likuwa linakaliwa na Jordan wakati wa vita vya mwaka 1967 vya masahariki ya kati na inadai kuwa mji huo wote ni wake.