rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Urusi Marekani Syria Iraq

Imechapishwa • Imehaririwa

Urusi yaishutumu Marekani kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa zamani wa IS

media
Marekani inasisitiza kuwa kambi ya Tanf ni kambi ya muda mfupi inayotumiwa kutoa mafunzo kwa vikosi vinavyotoa ushiriki wao kwa kupambana na wapiganaji wa IS. REUTERS/Erik De Castro

Mkuu wa majeshi ya Urusi ameishtumu Marekani kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa zamani wa kundi la Islamic (IS) nchini Syria ili kuhatarisha usalama wa nchi hiyo


Jenerali Valery Guerassimov amesema, katika mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la kila siku la Komsomolskaya Pravda, kwamba jeshi la Marekani linatumia kambi ya kijeshi ya Tanf, kambi kubwa kwa mawasiliano muhimu kwenye mpaka wa Iraq kusini mwa Syria.

Kambi hii iliotajwa kinyume cha sheria na eneo lilinaloizunguka vinaunda "shimo nyeusi" ambalo wapiganaji wa Kiiislamu wanaweza kuendesha mazoezi yao,Jenerali Guerassimov amebaini.

Marekani inasisitiza kuwa kambi ya Tanf ni kambi ya muda mfupi inayotumiwa kutoa mafunzo kwa vikosi vinavyotoa ushiriki wao kwa kupambana na wapiganaji wa IS.

Jeshi la Marekani limekanusha mara kadha tuhuma hizo dhidi yake.

Jenerali Guerassimov amesema kuwa wapiganaji hao wa zamani wa IS wanajiita Jeshi Jipya la Syria au wanatumia majina mengine.

Uwepo wa wapiganaji hawa katika kambi ya Tanf uligunduliwa na satelaiti pamoja na ndege zisizokuwa na rubani za Urusi. Jenerali Guerassimov ameongeza kuwa sehemu kubwa ya wanajihadi na askari wa zamani wa IS pia wako katika mji wa Chadadi,katika kambi nyingine ya Marekani.