Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-MAREKANI-HAMAS-USALAMA

Hamas yaonya dhidi ya mpango wa Marekani juu ya Jerusalem

Kiongozi wa kundi la Hamas katika Mamlaka ya Palestina Ismail Haniya, amedai kuwa Marekani ilikuwa imeipa Palestina eneo la Abu Dis kuwa makao makuu ya taifa lijalo la Palestina, ili kuachana na Jerusalem Mashariki.

Kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniya, (katikati) akihudhuria mkutano wa wakuu wake wa usalama mnamo Januari 13, 2011.
Kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniya, (katikati) akihudhuria mkutano wa wakuu wake wa usalama mnamo Januari 13, 2011. AFP PHOTO/MAHMUD HAMS
Matangazo ya kibiashara

Bw Haniya amewaambia wazee wa Kipalestina katika ukanda wa Gaza kuwa, mapngo huo wa Marekani unalenga kuimaliza Palestina.

Palestina imekasirishwa na hatua ya Marekani kutambua Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel.

Hayo yanajiri wakati ambapo mji wa Jerusalem unaendelea kutambuliwa na baadhi ya nchi washirika wa Marekani kama mji mkuu wa Israel.

Mapema wiki hii rais wa Guatemala Jimmy Morales, alitangaza nia yake ya kuhamisha ubalozi wa nchi yake nchini Israeli katika mji wa Jerusalem.

Katika kutaka kuhamisha ubalozi wa Guatemala kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem, rais Jimmy Morales alifuata msimamo wa Donald Trump na kuonyesha mafungamano yake na Washington, hata kama alieleza kwamba uamuzi wake unatokana na uhusiano mzuri wa nchi yake na Israeli.Tangazo hili halikuwashangaza wengi, kwa sababu Guatemala ni moja kati ya nchi tisa zilizounga mkono Marekani na Israeli wakati wa kura ya Alhamisi, Desemba 21, kuhusu azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Azimio hilo lilishtumu uamuzi wa Marekani kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa taifa la Kiyahudi.

Siku moja kabla ya mkutano huo rais Donald Trump alitishia nchi ambazo zitapigia kura azimio kuwachukulia vikwazo vya kifedha kutoka Marekani. Kwa sababu Guatemala inategemea kwa kiasi kikubwa msaada wa kiuchumi kutoka Marekani. Ni wazi kuwa rais Jimmy Morales amekubali kufanya hivyo shinikizo kutoka ikulu ya White House.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.