Pata taarifa kuu

Marekani na Saudi Arabia washtumiwa kufadhili kundi la IS

Ripoti ya shirika lisilo la kiserikali la Conflict Armament Research (CAR) inazishtumu Marekani na Saudi Arabia kufadhili kwa njia moja ama nyingne kundi la Islamic State.Silaha zilizotolewa na Marekani na Saudi Arabia kwa waasi nchini Syria zilichukuliwa moja kwa moja na kundi la Islamic State kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Bendera ya kundi la Islamic State kwenye barabara ya Al-Al-Fatiha inayoelekea kwenye kambi ya jeshi, kusini mwa Hawija, mnamo Oktoba 2, 2017.
Bendera ya kundi la Islamic State kwenye barabara ya Al-Al-Fatiha inayoelekea kwenye kambi ya jeshi, kusini mwa Hawija, mnamo Oktoba 2, 2017. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti hiyo iliyotolewa baada ya miaka mitatu ya utafiti kwenye maeneo ya kivita nchini Syria, shirika hilo lilichunguza kwa kina silaha zilizotumiwa na kundi la Islamic State, kulingana na sampuli ya vipande 40,000. "Ugavi wa kimataifa wa silaha kwa makundi ya waasi katika mgogoro wa Syria umeongeza kwa kiasi kikubwa wingi na ubora wa silaha kwa kundi la Islamic State (IS)," ripoti inasema.

Kulingana na ripoti ya CAR, Washington na Riyadh walitoa silaha, "inaonekana kwa vikosi vya upinzani vya Syria." Kwanza, shirika hili linaelezea kwamba Marekani haikuwa na haki ya kutuma kwa waasi hao silaha zilizopatikana kutoka kwa wauzaji wa Ulaya. Silaha hizo zilinunuliwa hasa nchini Romania na Bulgaria. Silaha hizo zilizotolewa kwa waasi nchini Syria zilianguka mikononi mwa kundi la Islamic State. Ripoti hiyo inasema kuwa hali hiyo "ilipelekea IS kupata kiasi kikubwa cha silaha kubwa za kivita".

Sio mara ya kwanza tukio kama hilo kutokea. Marekani, Ufaransa na Uingereza waliwahi kutoa silaha kwa vikosi vya upinzani vya Syria wakati vita vilipozuka nchini humo. Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Nusra (lenye mafungamano na Al Qaeda) lilichukua silaha hizo siku chache baadaye.

Kwa upande mwengine waasi wa waliopewa mafunzo na CIA nchini Jordan walitoroka kundi hilo la waasi na silaha zao na kujiunga na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu. Jambo ambalo lilipelekea Marekani kusitisha mpango wake wa kutoa mafunzo kwa waasi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.